Simba na Ngiri

Report 70 Downloads 115 Views
Simba na Ngiri Lion and Warthog South African Folktale Bilingual edition: Swahili & English

Hapo zamani za kale, Simba alikuwa mwenye nguvu na aliyeogopwa kuliko wanyama wote. Angeweza kuwashika wanyama wengine na kuwala. Lakini asubuhi moja alipokuwa akitafuta kifungua kinywa, alinaswa kwa mtego wa mwindaji. Once upon a time, Lion was the strongest and most feared of all the animals. He would catch other animals and eat them. But one morning while he was looking for his breakfast, he got caught in a hunter’s trap. 1

Simba alipiga yowe kubwa kutokana na uchungu. Alivuta na kuvuta ili kujinasua kutoka mtegoni. Mtego ulinasa zaidi na zaidi mguuni kila alipovuta. Simba alichoka na kuhisi uchungu mguuni. Alikata tamaa. Lion gave his loudest roar from the pain. He pulled and pulled to free himself from the trap. The trap got tighter and tighter around his leg every time he pulled. Lion grew tired and he felt more pain in his leg. Finally, he gave up. 2

Siku zilipita na Simba alichomwa kwa jua. Alikuwa na njaa na kiu na hakuwa na wakumwokoa. Alikuwa mnyonge zaidi na zaidi. “Nitakufa kwa njaa na kiu kwenye mtego huu,” aliwaza. Days went past as Lion sat baking in the sun. He was hungry and thirsty and there was nobody to save him. He became weaker and weaker. “I am going to die of hunger and thirst in this trap,” he thought to himself. 3

Asubuhi moja, Simba alisikia sauti ikitokea kichakani. Alisikiliza na kuchunguza kwa karibu. Aliona Ngiri akitembea na mkwewe na watoto wakizungumza na kucheka. Familia ya Ngiri ilikuwa inakwenda mtoni kunywa maji na kuchezea topeni kabla ya jua kuwa kali sana. One morning, Lion heard a sound coming from the nearby bushes. He listened and looked closer. He saw Warthog walking with his wife and children, talking and laughing. The Warthog family were going to the river to drink water and play in the mud before the sun got too hot. 4

“Ngiri! Tafadhali nisaidie! Ngiri!” Simba alilia. “Tafadhali niokoe kutoka mtego huu,” Simba alimsihi. “Kamwe,” Ngiri alijibu. “Wewe ni mnyama mkatili. Nikikuokoa utanila mimi na familia yangu kama kifungua kinywa.” “Naahidi kamwe sitatenda jambo ovu kama hilo. Tutakuwa marafiki ikiwa utaniokoa,” Simba alisema. “Warthog! Please help me! Warthog!” cried Lion. “Please set me free from this trap,” pleaded Lion. “Never,” said Warthog. “You are a cruel animal. You will eat me and my family for breakfast if I set you free.” “I promise I will never do such a bad thing. We will be friends if you can set me free,” said Lion. 5

Ngiri alimwonea Simba huruma. “Sipendi kukuona ukihisi uchungu, kiu na kuwa karibu kufa kwa njaa.” Kwa hivyo alitumia pembe zake akavuta mtego kisha akamwokoa Simba. Ngiri alimwokoa rafikiye mpya. Warthog felt sorry for the lion. “I do not like seeing you in such pain, thirsty and dying from hunger.” So he pulled at the trap with his long strong tusks and released Lion. Warthog saved his new friend. 6

“Asante sana rafiki yangu kwa kuokoa maisha yangu,” Simba alisema. “Lazima niende kwa familia yangu sasa, kwa heri.” “Nenda salama rafiki yangu,” Ngiri alijibu. Alifurahi kwamba Simba alikuwa rafiki yake. “Familia yangu haitakimbia kutoroka simba tena,” aliwaza. “Thank you very much my friend for saving my life,” said Lion. “I must go to my family now, good bye.” “Go well my friend,” said Warthog. He was happy that Lion was his friend. “My family will never have to run from the lion again,” he thought. 7

Simba aliondoka akichechemea na kwa unyonge. Vile vile alihisi njaa sana. Mara akawaona watoto wa Ngiri wakicheza topeni. “Leo ni siku yangu ya bahati,” Simba alisema akidondokwa na mate. Lion walked away limping and weak. He was also very hungry. Then he saw Warthog’s children playing in the mud. “Today is my lucky day,” said Lion with his mouth watering. 8

“Ngiri, rafiki yangu mpya,” Simba aliita. “Nimenaswa mtegoni kwa siku nyingi bila chakula. Lakini sina nguvu za kuwinda. Tafadhali, unaweza nipatia mmoja wa watoto wako kuwa kifungua kinywa changu?” Ngiri alishtuka. Nilikuokoa kutoka mtegoni na sasa unataka kula watoto wangu?” “Hey Warthog, my new friend,” called Lion. “I have been caught in the trap for days without food. But I am too weak to hunt. Please would you give one of your children to me for breakfast?” Warthog was shocked. “I saved you from the trap and now you want to eat my children?” 9

“Nasikitika rafiki yangu,” Simba alisema, “lakini ninakufa njaa. Ingawa mimi ni mnyonge sasa mimi ni mwenye nguvu kukuliko wewe.” Simba alifungua kinywa chake na kuonyesha meno yake. “Usiponipatia mmoja wa watoto wako, mwenyewe nitamchukuwa mmoja,” alinguruma. “I am very sorry my friend,” said Lion, “but I am starving. I might be weak for now but I am stronger than you.” The lion opened his mouth and showed his strong yellow teeth. “If you do not give me one of your children, I will take one for myself,” he roared. 10

Ngiri alifahamu kuwa hakuwa na mbio wala nguvu za Simba. Hangeweza kuwalinga wanawe katika vita. “Sawa sawa,” Ngiri alisema. “Nitakupatia mtoto wangu mmoja. Lakini kwanza hebu nionyeshe namna ulivyonaswa mtegoni. Ikiwa nitahitajika tena kumwokoa simba mwingine kutoka mtegoni.” Warthog knew that he did not have the speed or the strength of Lion. He would never be able to protect his children in a fight. “Al right,” said Warthog. “I will give you one of my children. But first I want you to show me how you were caught in the trap. In case I have to save another lion from this trap.” 11

Simba alifikiria juu ya utamu wa kumla ngiri mchanga. Hangeweza kusubiri. Simba alikwenda mtegoni na kuweka mguu wake ndani kumwonyesha rafiki yake jinsi alivyonaswa. Lion imagined the wonderful taste of young warthog in his mouth. He could hardly wait. Lion went back to the trap and put his foot inside to show his friend how he was trapped. 12

“Ouch!” Lion roared. “Ui!” Simba alinguruma. Ngiri alikaza mtego kwenye mguu wa simba. “Aha! Nimekupata,” Ngiri akasema. “Utakaa mtegoni kwa njaa na kiu tena. Tuone ikiwa meno yako makali na yenye nguvu yatakusaidia sasa.” “Ouch!” Lion roared. Warthog had closed the trap on Lion’s foot. “Aha! I got you,” said Warthog. “You will stay in that trap hungry and thirsty again. See if your strong teeth and sharp claws can help you now.” 13

“Kimbieni! Kimbilieni mbali!” Bibiye Ngiri aliwaambia wanawe kwa sauti ya juu. “Inueni mikia yenu mnapokimbia ili baba yenu awaone,” alisizitiza. Watoto walikimbia kwa kasi walivyoweza kupita kichakani. “Run! Run! Run away!” Warthog’s wife shouted to the children at the top of her voice. “Raise your tails when you are running so that your father can see you,” she called. The babies ran as fast as they could through the bushes. 14

“Tafadhali Ngiri nisaidie!” Simba alimsihi tena. Alihisi uchungu kwa kunaswa katika meno ya mtego wa mwindaji. “Nitakufanyia lolote utakalo ukiniokoa.” “La,sitathubutu, wewe ni muongo! Sitawahi kukwamini tena,” Ngiri alisema. “Nitawaonya wanyama wengine vile vile ili wakuepuke kwa sababu wewe ni mjanja mno. “Warthog please help me!” begged Lion again. He was in pain from the sharp jaws of the hunter’s trap. “I will do anything for you if you save me.” “No way, liar! I will never believe you again,” said Warthog. “I will also warn other animals not to save you because you are very sly.” 15

Ngiri aliwaona watoto wake wakikimbia katika mstari pamoja na mama yao. Mikia yao ilikuwa imeinuliwa juu ili awaone. Aliharakisha walipokuwa na wote wakakimbilia usalama wao. Hadi leo, Ngiri na watoto wao hukimbia huku mikia yao imeinuliwa kuhakikisha usalama wa kila mmoja wao. Warthog saw his children running in a row with their mother. Their tails were lifted up for him to see them. He rushed to his family and they all escaped to safety. To this day, Warthogs and their children always run with their tails lifted up to see that everyone is safe. 16

Text: South African Folktale Illustrations: Wiehan de Jager Translation: Brigid Simiyu Language: Swahili & English This story is brought to you by the Global African Storybook Project, an effort to translate the stories of the African Storybook Project into all the languages of the world. You can view the original story on the ASP website here

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 Unported License.